KLINSMANN AJIPA MATUMAINI BAADA YA KIPIGO CHA MEXICO.
KOCHA wa timu ya taifa ya Marekani, Jurgen Klinsmann amesema kikosi chake kilichukizwa na kusononeshwa na matokeo ya kufungwa mabao 2-1 na Mexico katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia uliofanyika Ijumaa usiku huo Columbus, Ohio. Mabao yaliyofungwa na Miguel Layun na Rafa Marquez yalitosha kuipa Mexico ushindi wao wa kwanza katika ardhi ya nchi hiyo toka mwaka 1972. Ushindi huo pia unaifanya Mexico kuanza vyema mechi zao za kufuzu kwa nchi za Amerika Kusini na Kati-CONCACAF. Akihojiwa Klinsmann amesema mechi zote za kufuzu huwa ni ngumu na ndio jinsi wachezaji wake walivyojiandaa, lakini wakicheza kama walivyofanya kipindi cha pili dhidi ya Mexico hakuna shaka kuwa wanaweza kupata matokeo mazuri huko mbele.
No comments:
Post a Comment