Monday, November 14, 2016

JUVENTUS YAMUWEKA DEPAY KATIKA RADA ZAKE.

KLABU ya Juventus inadaiwa kumuwinda winga wa Manchester United Memphis Depay kama ofa yao kwa ajili ya James Rodriguez ikikataliwa. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa hayupo katika mipango ya Jose Mourinho, huku Everton nao wakidaiwa kutaka kumsajili kumsajili kwa mkopo. Hata hivyo, Everton wanaweza kukabiliana na ushindani kutoka Juventus katika kipindi cha usajili. Mabingwa hao wa Serie A wanadaiwa kuwa tayari wameshapanga kumsajili Rodriguez katika usajili wa Januari lakini wanaweza kuhamia kwa Depay kama wakishindwa kumng’oa kiungo huyo Santiago Bernabeu. Rodriguez anaweza kuwagharimu Juventus paundi milioni 75 kwa mkataba wa moja kwa moja, lakini Depay anaweza kupatikana kwa mkopo kwasababu ya kuhitaji muda zaidi wa kucheza nje ya Old Trafford.

No comments:

Post a Comment