Monday, November 14, 2016

TAARIFA ZA GRIEZMANN ZAIPA AHUENI ATLETICO.

KLABU ya Atletico Madrid imethibitisha kuwa mshambuliaji wao Antoine Griezmann hakuvunjika mguu katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia kati ya Ufaransa na Sweden. Griezmann alitolewa nje katika kipindi cha kwanza katika ushindi wa mabao 2-1 iliyopata Ufaransa Ijumaa iliyopita baada ya kuumia mguu wake wa kushoto na baadae kutolewa kabisa kwenye kikosi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Ivory Coast kwa tahadhari. Baada ya kufanyiwa vipimo zaidi imegundulika kuwa nyota huyo alipata maumivu ya kawaida na aanaendelea na matibabu jijini Madrid huku akitarajiwa kupona kwa wakati kwa ajili ya mchezo wao wa derby Novemba 19 mwaka huu. Taarifa ya klabu hiyo imedai kuwa pande zote mbili zimefikia makubaliano kuwa Griezmann arejee Madrid kwa ajili ya matibabu, sehemu ambayo tayari ameshakabidhiwa kwa madaktari wanaomhudumia. Griezmann ameshafunga mabao nane na kusaidi mengine matano katika mechi 14 za mashindano yote alizocheza msimu huu.

No comments:

Post a Comment