Tuesday, November 22, 2016

MASHABIKI WA UNITED WAJIFICHA CHOONI KUONA MECHI DHIDI YA ARSENAL.

MASHABIKI wawili wa Manchester United walijificha na kulala katika choo cha Uwanja wa Old Trafford kwa madhumuni ya kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Arsenal uliochezwa Jumamosi iliyopita. Mashabiki hao walikuwa katika ziara ya kuutembelea uwanja huo lakini walifanikiwa kutoroka katika kundi ya watu waliokuwa wakitembezwa kuona maeneo mbalimbali ya uwanja huo. Hata hivyo, wawili hao walikamatwa Jumamosi asubuhi wakati wa ukaguzi wa usalama wa uwanja kabla ya kukabidhiwa mikononi mwa polisi ambao waliamua kutowachukulia hatua. Taarifa ya United imedai kuwa hakukuwa na hatari yeyote kwa mashabiki waliohudhuria mchezo huo dhidi ya Arsenal.

No comments:

Post a Comment