Tuesday, November 22, 2016

LEICESTER MBIONI KUANDIKA HISTORIA NYINGINE.

KLABU ya Leicester City baadae leo inaweza kuweka historia nyingine kwa kutinga hatua ya 16 ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kama wakiepuka kufungwa na Club Brugge. Leicester pamoja na kusuasua katika Ligi Kuu msimu huu, hali imekuwa tofauti Ulaya kwani ndio wanaongoza kundi G kwa tofauti ya alama tatu huku wakifanikiwa kuzuia nyavu zao kutikiswa katika mechi zote nne. Akihojiwa meneja wa Leicester, Claudio Ranieri amesema msimu uliopita walifanya kitu muhimu na msimu huu wanafanya kitu muhimu pia. Ranieri aliendelea kudai kuwa kutinga hatua ya timu 16 bora kwa mara ya kwanza katika historia yao ni mafanikio makubwa hivyo watajitahidi kufanya bidii ili kuhakikisha wanapata matokeo katika mechi zao zote mbili zilizobakia.

No comments:

Post a Comment