Wednesday, November 16, 2016

MESSI AWAONGOZA WACHEZAJI WECHEZAJI WENZAKE KUSUSIA MKUTANO WA WANAHABARI BAADA YA KUICHAPA COLOMBIA 3-0.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina, Lionel Messi amewaongoza wachezaji wenzake kususia kuzungumza na wanahabari baada ya kukosoa kiwango cha timu hiyo. Messi alitangaza mgomo huo baada ya kufunga bao katika ushindi wa mabao 3-0 waliopata dhidi ya Colombia katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia Alfajiri ya leo. Kituo kimoja cha redio nchini humo kiliripoti kuwa mshambuliaji Ezequiel Lavezzi alivuta bangi baada ya kufanya amzoezi, tuhuma ambazo alizikanusha vikali. Akiongeza kwa niaba ya wenzake, Messi aliyeingia katika mkutano wa wanahabari na kikosi chote cha wachezaji 25 wa timu hiyo, amesema wamepokea tuhuma nyingi na kukosewa heshima na hawajawahi kusema chochote.  Lionel Messi amewaongoza wachezaji wa timu ya taifa ya Argentina kususia kuongea na wanahabari baada ya uokosoaji kuhusu uchezaji duni wa timu hiyo. Messi aliendelea kudai kuwa anafahamu wanahabari wengi hawana heshima na mchezo huo lakini kuingilia maisha ya mtu binafsi ni jambo lisilokubalika. Pia imetangazwa kuwa Lavezzi anataka kumchukulia hatua za kisheria mtangazaji aliyesambaza tuhuma hizo.

No comments:

Post a Comment