MENEJA wa Manchester United, Jose Mourinho amesema ulikuwa ni uamuzi wa kitaalamu na kibinadamu kumruhusu kiungo Bastin Schweinsteiger kujiunga tena na kikosi cha kwanza kwa ajili ya mazoezi wiki hii. Nahodha huyo wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 32, alikuwa kifanya mazoezi mwenyewe au na vijana wa chini ya umri wa miaka 23 toka Mourinho achukue mikoba ya klabu hiyo majira ya kiangazi. Mara ya mwisho Schweinsteiger kuichezea United ilikuwa ni Machi mwaka huu, chini meneja aliyeondoka Louis van Gaal. Akihojiwa kueleka mchezo wao wa baadae leo wa Europa League dhidi ya Fenerbahce, Mourinho amesema Scheinsteiger amerejea na akiendelea kubaki nao anaweza kupata naafsi ya kucheza. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa kwasasa hana matatizo katika safu ya kiungo kama ilivyo katika safu ya ulinzi.
No comments:
Post a Comment