Thursday, November 3, 2016

ARTETA AMTUSI MESSI.

KOCHA msadizi wa Manchester City, Mikel Arteta anatuhumiwa kumtolea maneno ya matusi mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi katika mchezo baina ya timu hizo uliochezwa Jumanne iliyopita. Katika mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Etihad na City kushinda mabao 3-1, Arteta anadaiwa kuwa alimfuata Messi na kumwmabia maneno hayo wakati katika korido za kuingilia vyumba vya kubadilishia nguo. Kufuatia kauli hiyo, Messi anadaiwa kuwa alimjibu kiungo huyo wa zamani wa Arsenal kwa hasira. Arteta mwenye umri wa miaka 34, alianza kucheza soka lake katika klabu ya Barcelona lakini hakufanikiwa kucheza katika kikosi cha kwanza, na alistaafu mapema kiangazi baada ya kuitumikia Arsenal kwa miaka mitano.

No comments:

Post a Comment