MSHAMBULIAJI wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang aliachwa katika kikosi cha timu hiyo kilichokwaana na Sporting Lisbon jana kutokana na sababu za ndani. Aubameyang alitegemewa kuanza katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini hakutajwa kabisa katika kikosi cha wachezaji 18. Meneja wa timu hiyoThomas Tuchel na Ofisa Mkuu Hans-Joachim Watzke wote walithibitisha kuachwa kwa mchezaji huyo lakini wakasisitiza kuwa atarejea kikosini leo. Akihojiwa Tuchel amesema Aubameyang aliachwa kwa sababu za ndani hivyo hawezi kuweka hadharani sababu hizo kwasasa.
No comments:
Post a Comment