MSHAMBULIAJI nyota wa AS Monaco Radamel Falcao anatarajia kufunga mabao zaidi kwa klabu hiyo baada kumaliza ukame wa miaka sita katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kufunga bao kwenye mchezo dhidi ya CSKA Moscow. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30, alifunga mabao mawili katika kipindi cha kwanza katika ushindi wa mabao 3-0 waliopata katika Uwanja wa Louis II. Falcao ambaye bao lake la mwisho katika michuano hiyo alifunga wakati FC Porto mwaka 2010, ameonyesha kupata ahueni haswa katika kipindi ambacho anataka kurejea katika kiwango chake. Akihojiwa Falcao amesema anajisikia furaha kwani taratibu anarejea katika kiwango chake na ana matumaini ataendelea kufunga mabao zaidi kwa Monaco.
No comments:
Post a Comment