Thursday, November 3, 2016

POCHETTINO AKATAA KUULAUMU UWANJA WA WEMBLEY KWA KIPIGO.

MENEJA wa Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino amekataa kulaumu Uwanja wa Wembley kuwa ndio uliochangia kupoteza mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayer Leverkusen. Spurs walitandikwa bao 1-0 jana na sasa kuwa wamepoteza mechi zao zote za Ulaya katika uwanja huo msimu huu. Klabu hiyo inacheza mechi zake za nyumbani za Ligi ya Mabingwa Ulaya Wembley wakati uwanja wao wa White Hart Lane ukikarabatiwa. Akihojiwa Pochettino amesema tatizo kubwa lililochangia kupoteza mchezo huo liko kwao na sio Uwanja wa Wembley. Spurs kwasasa wanashikilia nafasi ya tatu katika kundi E nyuma ya AS Monaco na Bayer Leverkusen huku kukiwa kumebaki mechi mbili kabla ya kumalizika kwa hatua ya makundi.

No comments:

Post a Comment