Monday, November 21, 2016

NAPOLI KUMUWANIA ZOUMA JANUARI.

KLABU ya Napoli inadaiwa kuwa matumaini Chelsea wanaweza kuwaruhusu kumchukua kwa mkopo Kurt Zouma katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo Januari mwakani. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 bado anajiuguza baada ya kupata majeruhi mabaya ya goti katika mchezo wa Ligi Kuu waliokutana na Manchester United Februari mwaka huu. Zouma hajacheza mecho yeyote ya kimashindano chini ya meneja mpya Antonio Conte na tayari tumeshuhudia kina David Luiz, Gary Cahill na Cesar Azpilicueta wakionyesha kuelewana vyema katika safu ya ulinzi ya timu hiyo. Chelsea wanadaiwa kuwa wanaweza kumruhusu beki huyo kuondoka kwa muda mfupi Januari ili aweze kupata muda zaidi wa kucheza na Napoli wanataka kumsajili ili aweze kuziba nafasi ya Kalidou Koulibaly atakayekwenda kushiriki michuano ta Mataifa ya Afrika mapema mwakani.

No comments:

Post a Comment