NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi, Javier Mascherano na Neymar mapema leo wamesafiri pamoja kuelekea Belo Horizonte kwa ajili ya mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kati ya Argentina na Brazil. Wachezaji hao walisafiri pamoja wakitumia ndege binafsi ya Neymar, hata hivyo hakuzungumza na wanahabari waliokuwa uwanja wa ndege katika mji huo na badala yake kila mmoja alielekea katika hoteli ambayo timu zao zilifikia. Nyota hao wote walicheza katika mechi Barcelona walioshinda mabao 2-1 dhidi ya Sevilla Jumapili iliyopita, lakini watakuwa timu tofauti katika mchezo huo, Mascherano na Messi wakiitumikia Argentina huku Neymar akiitumikia Brazil. Mchezo huo ni muhimu sana kwa Argentina kwani wanashikilia nafasi ya sita katika msimamo wa nchi za kutoka ukanda wa Amerika Kusini-CONMEBOL. Brazil ndio anaongoza msimu huo akiwa na alama 21 baada ya kucheza mechi 10 na wanafuatiwa na Uruguay, Ecuador, Colombia na Chile. Timu nne pekee ndio zinaweza kufuzu michuano hiyo itakayofanyika nchini Urusi mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment