KIUNGO wa Paris Saint-Germain-PSG, Blaise Matuidi amebainisha kuwa anaifikiria ofa ya mkataba mpya kutoka katika klabu hiyo. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa alikuwa akihusishwa na tetesi za kuondoka Parc des Princes katika kipindi cha kiangazi huku Juventus ikitajwa kuwa ndio klabu iliyokaribia kumsajili. Matuidi amekiri kuwa alitaka kwenda Serie A lakini baada ya kufanya mazungumzo na meneja mpya wa PSG Unai Emery aliamua kubakia. Akihojiwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 29, amesema kwasasa wako katikati ya msimu na amefurahi kwa klabu kumpa ofa ya mkataba mpya. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa kwasasa anaisoma kwa makini ofa hiyo mpya aliyopewa kabla ya kutoa uamuzi baadae.
No comments:
Post a Comment