WAKALA wa Hector Bellerin amedai kuwa mteja wake huyo anatarajia kusaini mkataba mpya na Arsenal baada ya kufanyika kwa majadiliano zaidi. Chipukizi huyo wa kimataifa wa Hispania, ameimarika na kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha kwanza cha Arsene Wenger toka aliposaliwa akitokea Barcelona mwaka 2011. Wakati kukiwa na tetesi kuwa Barcelona wanataka kumrejesha mchezaji huyo ambaye ametokea katika akademi yao ya La Masia, wakala wake Albert Botines amedai kuwa mazungumzo juu ya mkataba mpya yanakaribia kukamilika. Akihojiwa Botines amesema bado wako katika mazungumzo kuhusu mkataba wa Bellerini lakini wanakaribia kufikia mwishoni. Wakala huyo aliendelea kudai kuwa mteja wake anafurahia kuwepo Arsenal na huo utakuwa mkataba wake wa nne katika klabu hiyo hivyo ni wazi amekuwa akiendelea kuimarika vyema.
No comments:
Post a Comment