MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema anaweza kuendelea kucheza kwa miaka 10 zaidi baada ya kusaini mkataba na klabu hiyo. Mkataba wa sasa wa nyota huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 31 ulikuwa unamalizika Juni mwaka 2018 lakini sasa anatarajiwa kuendelea kubakia hapo mpaka Juni mwaka 2021. Akihojiwa Ronaldo amesema mkataba huo mpya hautakuwa wa mwisho kwake kusaini kwani anadhani bado ana miaka 10 ya kuendelea kucheza soka. Naye rais wa Madrid, Florentino Perez amesema wanataka kuendelea kubaki na Ronaldo kwa kipindi kirefu kijacho. Ronaldo amefunga mabao 371 toka ajiunge na Madrid akitokea United mwaka 2009 na ameisaidia klabu hiyo kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili na moja la La Liga.
No comments:
Post a Comment