Friday, November 18, 2016

SCHWEINSTEIGER ASISITIZA KUPIGANIA NAFASI YAKE OT.

KIUNGO wa Manchester United, Bastian Schweinsteiger amesisitiza bado anajituma ili kupata nafasi katika kikosi cha timu hiyo pamoja na Jose Mourinho kumuondoa katika mipango yake. Nahodha huyo wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani aliambiwa mapema Agosti kuwa hatakuwa katika mipango ya meneja huyo na kulazimishwa kufanya mwenyewe kwa kipindi kirefu. Mourinho alimuita tena kiungo huyo kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza mwishoni mwa mwezi uliopita lakini bado anategemewa kuondoka klabuni hapo Januari huku klabu ya Chicago Fire ya Marekani ikitajwa kumuwania. Akihojiwa Shweinsteiger amesema kuwa malengo yake bado ni kucheza United na ataendelea kujituma kadri awezavyo mazoezini kwa matumaini ya kupewa tena nafasi.

No comments:

Post a Comment