Friday, November 11, 2016

UMTITI KUKAA NJE YA UWNAJA WIKI TATU.

BEKI wa Barcelona, Samuel Umtiti anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu. Taarifa zilizotumwa katika mtandao wa klabu hiyo zinadai kuwa Umtiti aliumia wakati akiwa mazoezini na kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa jana. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 nafasi yake imechukuliwa na Eliaquim Mangala katika kikosi cha Ufaransa ambacho kinatarajia kucheza Sweden baadae leo jijini Paris katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia. Umtiti anatarajiwa pia kuukosa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Ivory Coast utakaofanyika Lens wiki ijayo na pia kuna uwezekano mkubwa wa kuukosa mchezo wa Clasico dhidi ya Real Madrid utakaofanyika Camp Nou Desemba 3.

No comments:

Post a Comment