KLABU ya Manchester United inadaiwa kutaka kuachana na Bastian Scheinsteiger na wako tayari kupokea ofa ya paundi milioni 10 kwa ajili ya kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani Januari mwakani. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32, amekuwa hayuko katika mipango ya meneja Jose Mourinho na toka msimu umeoanza ametumia muda mrefu akifanya mazoezi na timu ya wachezaji wa akiba. Ingawa kwasasa kiungo huyo wa zamani wa Bayern Munich, amerejea kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza, hakuna uwezekano wowote wa kupangwa katika mechi. United sasa inadaiwa kuhaha kutafuta timu ambayo itakuwa tayari kumchukua kiungo huyo ambaye analipwa kitita cha paundi 180,000 kwa wiki.
No comments:
Post a Comment