RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter amemtuhumu mrithi wake Gianni Infantino kwa kutomuheshimu na kudai kuwa hapokei simu zake. Blatter mwenye umri wa miaka 80, amesema alikutana na Infantino kujadili maswali ambayo yalikuwa yakitaka majibu kwenye shirikisho hilo. Blatter aliendelea kudai kuwa Infantino alimuahidi kuwa atafanyia kazi lakini kamwe hajamrejeshea majibu na hapokei simu zake. Rufani ya Blatter kupinga kufungiwa miaka sita kujishughulisha na soka ilitupiliwa mbali mwishoni mapema wiki hii na Mahakama ya Michezo ya Kimataifa-CAS. Blatter amesema kamwe hafurahishwi na kinachoendelea FIFA na hajawahi kuona kampuni yeyote ambayo rais mpya anamdharau rais wa zamani.
No comments:
Post a Comment