KLABU ya Liverpool inajipanga kutuma ofa ya paundi milioni 18.5 kwa ajili ya kiungo wa Atalanta Franck Kessie. Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 19 amekuwa akizivutia klabu nyingi kubwa barani Ulaya zikiwemo Manchester City na Manchester United wakati Juventus nao wamepania kumbakisha Serie A. Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amekuwa akimhusudu sana nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ambaye aliitwa katika kikosi cha timu ya taifa akiwa na umri wa miaka 17. Hata hivyo, taarifa zinadai kuwa Liverpool watakabiliwa na vita kubwa pindi watakapotuma ofa hiyo kutokana na jinsi klabu nyingi zinavyomtaka nyota huyo.
No comments:
Post a Comment