KAMPUNI ya uwakala inayomsimamia Cristiano Ronaldo, Gestifute imetoa ushahidi zaidi kuonyesha kuwa nyota huyo wa Real Madrid amekuwa akilipa kodi zake zote. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno amekuwa akituhumiwa na vyombo kadhaa vya habari Ulaya kuwa amekuwa akikwepa kodi kupitia kampuni hiyo inayomilikiwa na wakala wake Jorge Mendes. Gestifute walikanusha taarifa hizo wiki iliyopita wakisisitiza kuwa mteja wao ni mlipa kodi mzuri na kutishia kuchukua hatua za kisheria kwa upande wowote unaosambaza taariafa hizo za uzushi. Baada ya Katibu Mkuu wa Hazina nchini Hispania, Jose Enrique Fernandez de Moya kukaririwa akidai kuwa atazifanyia uchunguzi taarifa hizo zilizotolewa, Gestifute wameamua kuweka wazi taarifa za mali na mikataba ya nyota huyo. Katika taarifa iliyotolewa jana jioni imeonyesha mali zote zenye thamani ya euro milioni 203 anazolimiki Ronaldo nchini humo pamoja na kuweka wazi mapato yote aliyopata mwaka jana.
No comments:
Post a Comment