Sunday, December 11, 2016

CITY WAMTENGEA ROSE PAUNDI MILIONI 25.

KLABU ya Manchester City inadaiwa kumtengea kitita cha paundi milioni 25 beki wa kushoto wa Tottenham Hotspurs Danny Rose. Meneja wa City Pep Guardiola anataka kusuka upya safu yake ya ulinzi kufuatia beki walionao kuwa wameshapita umri wa miaka 31 akiwemo Bacary Sagna, Pablo Zabaleta, Gael Clichy na Aleksander Kolarov. Taarifa zinadai kuwa Rose amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na maskauti wa City na wamekuwa wakipeleka taarifa nzuri kwa Guardiola na benchi lake la ufundi. Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza pia anawindwa na Manchester United.

No comments:

Post a Comment