Monday, December 5, 2016

LEWANDOWSKI KUONGEZA MKATABA BAYERN.

MSHAMBULIAJI nyota wa Bayern Munich, Robert Lewandowski anadaiwa kukaribia kufikia makubaliano ya mkataba mpya ambao utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika klabu hiyo. Mark Barthel ambaye anafanya kazi na wakala wa Lewandowski, Cezary Kucharsky amebainisha kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 anatarajiwa kuongeza mkataba wake. Barthel amesema haitachukua muda mrefu kabla ya Lewandowski hajasaini mkataba mpya. Mkataba wa sasa wa Lewandowski unamalizika mwka 2019, lakini Bayern wanataka kuona nyota huyo wa kimataifa wa Poland akiongeza mkataba mwingine.

No comments:

Post a Comment