NAHODHA wa Arsenal, Per Mertesacker amerejea mazoezini kuelekea mchezo wao wa mwisho wa kundi A wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC basel kesho. Beki huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 32 hajacheza mechi yeyote msimu huu baada ya kuumia goti wakati wa maandalizi ya msimu. Mapema leo Matersacker alionekana akikimbia huku akisimamiwa na mwalimu wa mazoezi Graig Gant wakati timu hiyo ikijiandaa na mchezo wao huo utakaofanyika Uswisi kesho usiku. Mustakabali wa beki huyo mzoefu unadaiw akuwa mashakani pindi mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa smimu huu, kufuatia Mjerumani mwenzake Shkodran Mustafi kuonekana kuliziba vyema pengo lake.
No comments:
Post a Comment