Monday, December 5, 2016

OZIL, SANCHEZ WAMUUMIZA KICHWA WENGER.

NYOTA wa Arsenal, Mesut Ozil na Alexis Sanchez wanadaiwa kutaka kulipwa mshahara sawa kama anaopata Paul Pogba katika klabu ya Manchester United. Nyota hao wote wamebakisha miezi 18 katika mikataba yao ya sasa na wamekuwa katika mazungumzo ya mikataba mipya huku mishahara ikiwa jambo kubwa linalojadiliwa. Ozil anapokea kitita cha paundi 140,000 kwa wiki wakati Sanchez yeye anakunja kiasi cha paundi 130,000 kwa wiki na wote wanadhani kwa mchango wao mkubwa wanaotoa katika klabu hiyo wanapswa kulipwa zaidi. Pogba ndiye mchezaji anayelipwa zaidi katika Ligi Kuu akikunja kitita cha paundi 290,000 kwa wiki, lakini Arsenal wanadaiwa hawatakuwa tayari kutoa zaidi ya paundi 200,000 kwa nyota wake hao.

No comments:

Post a Comment