Monday, December 5, 2016

ERIKSSON AENDA KUINOA TIMU YA DARAJA LA PILI CHINA.

KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Sven-Goran Eriksson ameteuliwa kuinoa klabu ya daraja la pili ya China Shenzhen FC akichukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Clerence Seedorf. Shenzhez mabingwa wa Ligi Kuu ya China mwaka 2004, walishindw akupanda daraja chini ya Seedorf msimu uliopita. Hatua hiyo imepelekea kocha huyo wa zamani wa AC Milan kutimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na mzoefu Eriksson. Eriksson mwenye umri wa miaka 68, ameamua kuchukua mikoba ya kuinoa timu hiyo ya daraja la chini baada ya kuwa amewahi kuzinoa timu za Ligi Kuu ikiwemo Guangzhou R&F na Shanghai SIPG. Aliondoka Shanghai Novemba mwaka jana baada ya timu hiyo kumalizika katika nafasi ya tatu na nafasi yake kuchukuliwa na Andre Villas Boas.

No comments:

Post a Comment