MENEJA wa Manchester United, Jose Mourinho ametetea uamuzi wake wa kumuingiza kiungo Marouane Fellaini katika mchezo wa jana ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1. Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alisababisha penati muda mchache baada ya kuingia katika dakika 85 na kupelekea Everton kufanikiwa kusawazisha. Akihojiwa Mourinho alitetea uamuzi wake wa kumuingiza kiungo huyo na kudai kuwa ulikuwa wa kiufundi kulingana na mchezo huo uliovyokuwa ukiendelea. Fellaini alichukua nafasi ya Henrikh Mkhitaryan dakika chache kabla ya kumchezea vibaya Idrissa Gueye na kupelekea Leighton Baines kusawazisha.
No comments:
Post a Comment