Thursday, December 8, 2016

LUNINGA ZA VIWANJANI KUSAIDIA WAAMUZI KWENYE MICHUANO YA KLABU BINGWA YA DUNIA.

WAAMUZI wanatarajiwa kuwezeshwa kutumia luninga zilizopo uwanjani kwa mara ya kwanza ili kuhakiki maamuzi yao wakati michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia itakapoanza kutimua vumbi nchini Japan baadae leo. Waamuzi watakaokuwa wakifuatilia mchezo katika luninga watakuwa wakipitia baadhi ya matukio kabla ya kumuarifu mwamuzi aanayekuwepo uwanjani. Mwamuzi baadae atapata nafasi ya kupitia tukio kwa baadhi maamuzi kitu ambacho hakikuruhusiwa katika majaribio yaliyopita. Ofisa wa maendeleo ya ufundi ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Marco van Basten amesema hatua ni muhimu sana na inaleta matumaini chanya.

No comments:

Post a Comment