Thursday, December 8, 2016

HATMA YA KUONGEZEKA KWA TIMU KOMBE LA DUNIA KUJULIKANA JANUARI.

MICHUANO ya Kombe la Dunia ijayo inatarajiwa kuwa na makundi 16 huku kukiwa na nchi tatu katika kila kundi kwenye timu 48 zitakazokuwepo kama ombi la rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Gianni Infantino likikubalika. Infantino ambaye amekuwa kiongozi wa FIFA Februari mwakani, huko nyuma amezungumzia kuiongeza michuano ya Kombe la Dunia kutoka timu 32 hadi 40. Chini ya mfumo wake wa makundi 16 timu mbili za juu ndio zitafuzu katika hatua ya timu 32 bora na kuendelea na hatua ya mtoano. Uamuzi unatarajiwa kufanyika Januari mwakani lakini mabadiliko yeyote yanaweza kuja kuanza kufanya baada ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2026. Baraza la FIFA linatarajia kusjadili ombi hilo Januari 9 mwakani.

No comments:

Post a Comment