Thursday, December 8, 2016

MADRID YAFIKIA REKODI YA KUTOFUNGWA MECHI 34 ILIYOWEKWA MIAKA 27 ILIYOPITA.


KLABU ya Real Madrid imefikia rekodi ya kutofungwa mechi 34 kufuatia sare ya mabao 2-2 dhidi ya Borussia Dortmund katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana. Hata hivyo, matokeo hayo hayakutosha kuifanya Madrid kufuzu hatua ya timu 16 bora wakiwa vinara wa kundi F baada ya kuzidiwa na wapinzani wao Dortmund. Madrid walionekana kumudu vyema mchezo kufuatia mabao mawili mawili yaliyofungwa na Karim Benzema lakini mambo yalibadilika baada ya mabao ya kusawazisha Pierre-Emerick Aubameyang na Marco Reus. Kipigo chao cha mwisho kilikuwa ni mabao 2-0 walichopata kutoka kwa Wolfsburg katika michuano hiyo Aprili 6 msimu uliopita na toka wakati huo wamepata ushindi katika mechi 24 na kutoa sare tisa katika mashindano yote huku wakifunga mabao 94 na kuungwa 31 pekee. Rekodi ya kucheza mechi 34 bila kufungwa awali iliwekwa na timu ya Leo Beenhakker katika msimu wa 1988-1989 ambapo walikwenda na kushinda taji la Primera Division wakipoteza mechi moja kati ya 38.

No comments:

Post a Comment