Thursday, December 8, 2016

SHAKHTAR YKIRI BARCELONA INAMUWANIA SRNA.

MENEJA wa Shakhar Donetsk, Paulo Fosesca amekiri Barcelona inamuwania beki wao wa kulia Darijo Srna lakini amesisitiza ana matumaini klabu hiyo kongwe nchini Ukraine itambakisha nahodha wake huyo. Nyota huyo wa kimataifa wa Croatia amekuwa akihusishwa na tetesi za kwenda kwa mabingwa hao wa La Liga kufuatia wasiwasi wa mustakabali wa Aleix Vidal Camp Nou. Srna ameitumikia Shakhtar toka mwaka 2003 na Fonsesca ana matumaini kuwa beki huyo mwenye umri wa miaka 34 ataendelea kubakia pamoja na kuwindwa na Barcelona. Akihojiwa kuelekea katika mchezo wa Europa League dhidi ya Sporting Braga baadae leo, Fosesca amesema anafahamu kuwa Barcelona wanamuwania Srna lakini ana matumaini beki huyo atabakia kutokana na umuhimu wake kwao.

No comments:

Post a Comment