Thursday, December 8, 2016

MMOJA WA MANUSURA WA AJALI YA NDEGE YA CHAPECOENSE AANZA MAZOEZI.

BEKI wa Chapecoense, Alan Ruschel ametuma ujumbe wa video kwa mashabiki wakati akipiga hatua yake ya kwanza toka alipopata ajali ya ndege. Beki huyo mwenye umri wa miaka 27 ndio mtu wa kwanza kutolewa hai katika mabaki ya ajali ya ndege ambayo yalichukua maisha ya watu 71, wakiwemo wachezaji wenzake 19 wa Chapecoense. Ruschel alituma picha za video hiyo akiwa katika hospitali ya Somer nchini Colombia ambako anaendelea na matibabu. Katika ujumbe aliotuma na video hiyo, Ruschel aliwaambia mashabiki kuwa anaendelea vyema na anatarajia kurejea nchini Brazil kwa ajili ya kuendelea na matibabu zaidi huku akiwashukuru kwa maombi yao.

No comments:

Post a Comment