Thursday, December 8, 2016

PSG YAMUWANIA BEKI WA WOLFSBURG.

KLABU ya Paris Saint-Germain-PSG inadaiwa kuanza mazungumzo na beki wa kushoto wa Wolfsburg Ricardo Rodriguez. Arsenal na Chelsea nazo zimewahi kutajwa huko nyuma kumuania nyota huyo wa kimataifa wa Uswisi mwenye umri wa miaka 24 sambamba na Inter Milan na AC Milan. Chelsea na Arsenal walidhaniwa kukaribia kukamilisha usajili wake majira ya kiangazi lakini sasa upepo umehamia kwa PSG ambao wanadaiwa kuwa wameshaanza mazungumo naye. Wolfsburg hawataki kumuacha Rodriguez aondoke hata hivyo, wanaweza kumuachia endapo itapatikana timu itakayoweza kufikia thamani yake ya paundi milioni 21 iliyowekwa katika mkataba wake.

No comments:

Post a Comment