Thursday, December 8, 2016

SUAREZ KUONGEZA MKATABA BARCELONA.

RAIS wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu amedai kuwa Luis Suarez anatarajia kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay atasaini mkataba huo wa miaka sita ikiwa imepita miezi miwili toka mchezaji mwenzake Neymar asaini mkataba mpya wa mpaka 2021. Javier Mascherano na Ivan Rakitic nao pia tayari wameshasaini mikataba mipya huku Lionel Messi akitajwa kufuatia. Akihojiwa Bartomeu amesema tayari wameshamaliza mazungumzo na Suarez na kinachosubiriwa ni yeye kusaini mkataba huo mpya mwishoni mwa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment