CLAUDIO Ranieri, Fenarndo Santos na Zinedine Zidane ni miongoni mwa majina yaliyotajwa na Shirikisho la Soka Dunia-FIFA kwa ajili ya kugombea tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka. Mshindi wa mwisho anatarajiwa kuchaguliwa kwa kura zitakazopigwa na manahodha wa vikosi vya timu ya taifa pamoja na mashabiki watakaopiga kura zao mitandaoni na mshindi atakabidhiwa tuzo yake Januari mwakani. Ranieri ameingia katika orodha hiyo kufuatia kuiongoza Leicester City kutwaa taji la Ligi Kuu msimu uliopita huku Santos yeye akiiongoza Ureno kutwaa taji la michuano ya Ulaya huko Ufaransa majira ya kiangazi. Kwa upande wa Zidane yeye aliiongoza Madrod kutwaa taji lake la 11 la michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita. Luis Enrique, Diego Simeone, Chris Coleman, Jurgen Klopp, Mauricio Pochettino, Didier Deschamps na Pep Guardiola pia walikuwepo katika orodha hiyo kabla ya haijapunguzwa na kubakiwa makocha watatu.
No comments:
Post a Comment