Friday, December 2, 2016

MAN UNITED WAMUWANIA RAKITIC.

KLABU ya Manchester United inadaiwa kumuwania kiungo wa Barcelona Ivan Rakitic. Kiungo huyo wa kimataifa wa Croatia amekuwa akipata nafasi ya mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha Barcelona katika miezi ya karibuni na sambamba na Andres Iniesta na Sergio Busquets wamekuwa akitengeneza safu nzuri ya kiungo. Hata hivyo, uwepo wa Denis Suarez unatishia nafasi ya Rakitic na Jose Mourinho anataka kutumia mwanya huo kumchukua kiungo huyo ili aweze kucheza sambamba na Paul Pogba Old Trafford. Kwasasa taarifa zinadai kuwa Mourinho anajipanga kutoa ofa kwa ajili ya kiungo huyo ambaye mkataba wake Camp Nou unamalizika mwaka 2019.

No comments:

Post a Comment