Friday, December 2, 2016

KLOPP "AWAZODOA" WANAOMNYEMELEA STURRIDGE.

MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amepuuza tetesi zilizozunguka mustakabali wa Daniel Sturridge na kuweka wazi kuwa klabu hiyo haina mpango wa kuuza mchezaji yeyote wa kikosi cha kwanza Januari mwakani. Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza, ambaye anajiuguza majeruhi ya mguu, ameanza katika mechi tano pekee msimu huu huku Roberto Firmino akifanywa ndio mshambuliaji kiongozi wa klabu hiyo. Hatua hiyo imepelekea kuzuka tetesi kuwa muda wa Sturridge kuendelea kuwepo Anfield unaelekea ukingoni. Hata hivyo, tetesi hizo zimekanushwa na Klopp akidai kuwa vyombo vya habari vimekuwa vikitengeneza habari na kwamba nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 hata kwenda popote.

No comments:

Post a Comment