RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Gianni Infantino mapema leo ameahirisha safari ziara yake nchini Australia ili aweze kuhudhuria shughuli za mazishi za wachezaji waliofariki katika ajali ya ndege katika milima ya Colombia. Infantino ilikuwa atue jijini Sydney Jumatatu ijayo baada ya kushuhudia fainali ya Kombe la Dunia ya wanawake chini ya umri wa miaka 17 huko Papua New Guinea. Ndege iliyokuwa imewabeba wachezaji wa timu ya Chapecoense ya Brazil ilianguka karibu na mji wa Medellin nchini Colombia wakati wakiwa safarini kuelekea katika fainali ya Copa Sudamericana dhidi ya Atletico Nacional. Watu 71 waliokuwepo katika ndege hiyo walifariki dunia, wakiwemo wachezaji wa timu hiyo na waandishi 20 waliosafiri nao na watu sita pekee ndio waliopona.
No comments:
Post a Comment