Friday, December 2, 2016

WENGER KUTOZIBA NAFASI YA CAZORLA JANUARI.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa hana mpango wowote wa kutafuta mbadala wa Santi Cazorla Januari mwakani pamoja na kiungo huyo kupata majeruhi ya muda mrefu. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa miezi miwili mpaka mitatu pindi atakapofanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu na Wenger anadhani ana wachezaji wengi katika kikosi chake wanaoweza kuziba nafasi yake. Akihojiwa meneja huyo amesema ana viungo wa kutosha katika kikosi chake hivyo hatasajili mchezaji yeyote kuziba nafasi ya Cazorla katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo. Pamoja na hayo, Wenger amedai kuwa taarifa za Cazorla kuhitaji kufanyiwa upasuaji ni mbaya kwa kikosi chake lakini watajitahidi kadri wawezavyo kuhakikisha nafasi yake inazibwa vyema.

No comments:

Post a Comment