Friday, December 2, 2016

TIMU KUSIMAMA DAKIKA MOJA KUOMBOLEZA MWISHONI MWA WIKI.

KILA mechi itakayochezwa mwishoni mwa wiki hii wachezaji watasimama kwa dakika moja kuwakumbuka wachezaji na viongozi wa klabu ya Chapecoense ambao walifariki dunia katika ajali ya ndege Jumatatu. Shirikisho la Soka Duniani-FIFA pia limewataka wachezaji wote kuvaa vitambaa vyeusi mkononi katika kumbukumbu hiyo. Wachezaji 19 na benchi la ufundi ni miongoni mwa watu 71 ambao walifariki wakati ndege iliyokuwa imebeba timu hiyo ilipoanguka. Timu hiyo ilikuwa ikisafiri kwenda nchini Colombia kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Copa Sudamericana, ukiwa ni mchezo mkubwa katika historia ya klabu hiyo. Wiki ijayo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League, pia timu zitasimama kwa dakika moja.

No comments:

Post a Comment