Wednesday, November 30, 2016

HOENESS AMTAKA LAHM KUENDELEA KUCHEZA.

RAIS wa Bayern Munich, Uli Hoeness amesisitiza kuwa nahodha Philipp Lahm bado ni mchezaji muhimu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kufuatia tetesi kuwa anaweza kustaafu mwakani. Tetesi zimeibuka kuwa beki huyo wa kimataifa wa Ujerumani anatarajiwa kupewa nafasi ya ukurugenzi wa michezo wa klabu hiyo kama akitundika daruga zake mwishoni mwa msimu huu. Hata hivyo, Hoeness anataka Lahm amalize mkataba wake ambao utaishia mwaka 2018 kabla ya hajafikiria kibarua kingine Allianz Arena. Hoeness ambaye alichaguliwa tena kuiongoza Bayern wiki iliyopita, amesema anadhani Lahm bado ni mchezaji mzuri awapo uwanjani ana angependa amalize kwanza mkataba wake ndio afikirie suala la kustaafu.

No comments:

Post a Comment