KLABU ya Real Madrid mapema leo imefanikiwa kutwaa taji lake la pili katika kipindi cha miaka mitatu baada ya kuichapa Kashima Antlers ya Japan katika mchezo wa fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia. Katika mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Nissan jijini Yokohama Madrid walipata bao la mapema kupitia kwa Karim Benzema lakini wenyeji walicharuka na na kusawazisha bao hilo kabla ya mapumziko kupitia kwa nyota wao Gaku Shibasaki. Kipindi cha pili Kashima walipata bao lingine kupitia kwa Shibasaki kabla ya Cristiano Ronaldo hajasawazisha bao hilo kwa penati na kupelekea mchezo huo kwenda kwenye muda wa nyongeza. Ronaldo alifunga mabao mengine mawili kwenye muda wa nyongeza na kuweka historia mpya ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick katika historia ya michuano hiyo. Ushindi huo pia unafanya timu za Ulaya kutwaa taji hilo mara tisa kati ya 10.
No comments:
Post a Comment