Tuesday, December 20, 2016

LEICESTER WAIKATIA RUFANI KADI YA VARDY.

KLABU ya Leicester City imekata rufani kupinga kadi nyekundu alioonyeshwa mshambuliaji wao Jamie Vardy katika mchezo wa Jumamosi iliyopita uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Stoke City. Vardy alilimwa kadi hiyo katika dakika ya 28 baada ya kumkwatua kwa miguu miwili Mame Diouf. Kama rufani hiyo ikikataliwa nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza atatumikia adhabu ya kutocheza mechi tatu hivyo kukosa mechi dhidi ya Everton, West Ham United na Middlesbrough. Mabingwa hao wa Ligi Kuu wamesema kuwa wanatarajia kusikia matokeo ya rufani yao katika siku za karibuni.

No comments:

Post a Comment