MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte amedai kuwa ratiba yao ya msimu wa sikukuu inakosolewa kwasababu wako kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu. Chelsea wana nafasi kubwa ya mapumziko katika ratiba yao kuliko timu yeyote kwenye kipindi hiki huku meneja wa Manchester United Jose Mourinho naye akitoa kauli kuhusiana na faida inayopata klabu yake hiyo ya zamani. Chelsea wameshinda mechi 13 mfululizo katika ligi na wanaweza kufikia rekodi iliyowekwa na Arsenal mwaka 2002 kama wakifanikiwa kuichapa Tottenham Hotspurs baadae leo. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Conte alikiri kuwa ni kweli wana faida kidogo kwani wamepata muda wa kupumzika siku moja zaidi ya wapinzani wao Spurs lakini sio wao waliopanga ratiba. Conte aliendelea kudai kuwa anadhani malalamiko yamekuwa makubwa zaidi kwao kwasababu wanaongoza msimamo wa ligi.
No comments:
Post a Comment