KIUNGO wa Arsenal, Francis Coquelin anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki nne baada ya kuumia msuli wa paja wakati wa mchezo wa Ligi Kuu waliotoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Bournemouth juzi. Kuumia kwa kiungo huyo kunamuacha meneja Arsene Wenger kuwa na upungufu ya wachezaji wa viungo wa kati kufuatia kukosekana kwa Santi Cazorla anayeuguza majeruhi ya kifundo cha mguu na Mohamed Elneny aliyeitwa Misri kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika. Viungo pekee wa kati alionao kwasasa ni Aaron Ramsey na Granit Xhaka. Akiongea na wanahabari mapema leo Wenger alithibitisha taarifa za kumkosa beki huyo kwa kipindi cha mwezi mmoja huku akiongeza kuwa mshambuliaji Danny Welbeck anaweza kurejea tena uwanjani katika mchezo wa mzunguko wa tatu wa Kombe la FA dhidi ya Preston North End Jumamosi hii.
No comments:
Post a Comment