Thursday, January 5, 2017

HULL CITY WAMCHUKUA KOCHA WA ZAMANI WA OLIMPIAKOS.

MENEJA wa zamani wa Olympiakos, Marco Silva amethibitishwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Hull City. Meneja huyo mwenye umri wa miaka 39 raia wa Ureno, amesaini mkataba wa mpaka mwishoni mwa msimu na klabu hiyo yenye maskani yake katika Uwanja wa KCOM. Silva anachukua nafasi ya Mike Phelan aliyetimuliwa juzi kufuatia timu hiyo kuburuza mkia katika msimamo wa Ligi Kuu. Silva aliondoka Olympiakos kiangazi mwaka jana na alikuwa akihusishwa na tetesi za kuwindwa na klabu Championship ikiwemo Wolves na Nottingham Forest. Kibarua chake cha kwanza kitakuwa ni katika mchezo wa mzunguko wa tatu wa Kombe la FA dhidi ya Swansea City Jumamosi hii.

No comments:

Post a Comment