RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Gianni Infantino amekingia kifua kifua uamuzi wa kuongeza timu kufikia 48 katika michuano ya Kombe la Dunia akisisitiza uamuzi huo ulikuwa wa kimichezo na sio kutengeneza fedha. Kamati ya utendaji ya shirikisho hilo ilipiga kura kupitisha uamuzi huo wa mabadiliko katika mkutano uliofanyika jijini Zurich jana. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Infantino amesema uamuzi huo ulikuwa wa kimichezo zaidi kuliko fedha kama baadhi ya wadai wanavyodhani. Mabadiliko hayo mapya yatakuwa na makundi 16 yenye timu tatu ambapo timu mbili za juu zitasonga mbele katika hatua ya mtoano ya timu 32 bora na unaweza kuanza kutumika katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2026.
No comments:
Post a Comment