WACHEZAJI wa timu ya taifa ya Guinea-Bissau wamemaliza mgomo wao baada ya kulipwa posho zao, siku nne kabla ya kuanza kwa michuano ya Mataifa ya Afrika. Baada ya taarifa hizo kusambaa, maelfu ya wananchi walikusanyika katika mitaa ya mji mkuu wa Bissau kushuhudia maandamano ya kikosi hicho jana. Guinea-Bissau wanatarajiwa kucheza mchezo wa ufunguzi wa kundi A dhidi ya wenyeji Gabon Jumamosi hii. Pia watacheza na Burkina Faso na Cameroon katika hatua hiyo ya makundi. Kikosi hicho kilikuwa hakijalipwa stahiki zao kwa kufanikiwa kufuzu michuano hiyo hatua ambayo ilipelekea maandamano hayo.
No comments:
Post a Comment