Wednesday, January 11, 2017

ARSENAL WALISHINDWA BEI KWA BEKI LA ROMA.

WAKALA wa beki Kostas Manolas amedai kuwa klabu ya AS Roma ilikataa kitita cha euro milioni 40 kutoka Arsenal ili kumnasa nyota huyo msimu huu. Arsenal walikuwa wakihusishwa na usajili wa beki huyo katika kipindi cha usajili wa kiangazi mwaka jana lakini suala lake halikufanikiwa baada ya kumchukua Shkodran Mustafi kutoka Valencia badala yake. Wakala wa beki huyo amesisitiza kuwa kiasi cha fedha walichokitaka Roma ndio kilikuwa chanzo kikubwa cha kuvurugika kwa dili hilo. Hata hivyo wakala huyo aliendelea kudai kuwa Kostas anaweza kuondoka Juni mwaka huu ingawa ameondoa uwezekano wa kwenda China.

No comments:

Post a Comment